Sambaza

50 Cent Amjibu Hivi Ja Rule

HUENDA  hii ikawa ni wiki ya matukio kibao mtandaoni. Mapema jana msanii nguli wa hip hop Ja Rule aliweka wazi wakati anawasiliana na swizz beatz kwenye “instagram live” kuwa yupo tayari kupambanishwa na 50 Cent.

50 Cent hajakawia kumjibu Ja Rule na leo hii Aprili 14 ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika maneno ya kejeli kwa kusema “nani anataka kushindana? Na huu ndio wakati wa ukimya.” Akiwa anamaanisha wakati wa kumuaga/kutoa heshima kwa marehemu.

Hakuishia hapo, 50 Cent aliweka picha nyingine kwenye ukurasa huohuo ikimuonyesha Ja Rule akiwa kama ombaomba aliyeshika bango lililoandikwa “nitapambana na 50 Cent nipate kiki” kisha 50 Cent akaambatanisha na neno moja tu “mjinga.”

Ikumbukwe tu wawili hawa ni mahasimu wa muda mrefu na mashabiki wana hamu kuona kama ugomvi wao wa miaka ya 2000 utarudi tena au la.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey