Sambaza

Fabulous: Sipendi 2 Chainz Anavyochagua wa Kushindana naye

MAREKANI kwa sasa wapo kwenye kipindi ambacho kila mtu yupo ndani kwa kutii agizo la serikali ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa Corona lakini wasanii na wadau wa muziki wamepata namna ambayo itawaburudisha hukohuko majumbani na ni kwa kushindanisha wasanii wawili kwenye instagram live.

Mashindano hayo yamekuwa maarufu sana na 2 Chainz naye anataka kupata wa kushindana naye na alionekana akichagua baadhi ya wasanii anaotaka kushindana nao na kuwaacha wengine.

Kitendo hicho kimeonekana kumkera msanii nguli Fabulous ambaye aliweka wazi hayo akiwa anafanya mahojiano ambapo alijibu swali la kama yupo tayari kwa mashindano hayo kwa kusema “nipo tayari kufanya hivyo kirafiki, ila sijaona jina langu likitajwa mara kwa mara nimeona tu likishindanishwa na 2 Chainz ambaye sikupendezwa naye kuchagua wa kushindana naye.”

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey