Sambaza

Haya Ndiyo Majibu ya Alikiba Kwa Killy na Cheed…

BAADA ya Killy na Cheed ambao walikuwa wasanii wa Alikiba chini ya mwamvuli wa Kings Music kutangaza kuwa wamejiondoa rasmi kwenye lebo hiyo, huenda maneno aliyoandika Alikiba kwenye ukurasa wake wa instagram ndiyo majibu yake kwao.

Imemchukua Alikiba masaa takribani sita kuwajibu (kama hayo ndiyo majibu) kwa kuandika “unapomtendea mtu jambo lake tena kwa mapenzi yote, usitarajie fadhila wala malipo baadaye  kwa sababu kuna aina nyingi za binadamu ambapo si wote wenye moyo kama wako.”

Wadau wa muziki Tanzania bado wanajaribu kuunganisha nukta ili anagalau kupata picha halisi iliyosababisha wasanii hawa kujiondoa kwenye lebo hiyo.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey