Sambaza

Kayumba: Sijawahi Kuiona Milioni 50 ya BSS

Msanii ambaye ni miongoni mwa mazao ya Bongo Star Search yanayofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki Tanzania Kayumba amefunguka mengine mapya kuhusiana na shindano hilo.

Akiwa anafanya mahojiano na Given Mashishenga wa Global Tv Online, msanii huyo baada ya kuulizwa kuhusu sakata la washindi kutopewa stahiki zao na uongozi wa shindano hilo alijibu kwa kusema “Inasemekana kuwa waliweka pesa kwenye akaunti yangu ya benki, lakini kwa sababu nilikuwa mdogo kiumri hivyo akaunti ile ilkuwa ikiendeshwa na meneja Chambuso.”

Kayumba aliendelea kusema “zawadi pekee niliyoipata mikononi ni gari ambalo nalo nililetewa sio kwamba nilienda kulichukua mwenyewe na pia nyumba niliambiwa kuwa imeanza kujengwa hivyo niimalizie, nikawa naambiwa pesa zinatoka kwenda kuendeleza hiyo nyumba.”

Given hakusita kutaka udadavuvi wa nyumba aliyoambiwa amalizie na msanii huyo alijibu “nyumba niliimalizia lakini siwezi kusema ni yangu sababu sijakabidhiwa hati miliki na nimejaribu kufatilia naambiwa nifatilie mwenyewe.”

Hata hivyo Kayumba alisisitiza kuwa hawezi kumlaumu Madam Rita sababu hana uhakika labda alitoa hela ila kukawa na mtu wa kati aliyezifanyia ujanja ujanja au labda hakutoa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey