Sambaza

Keri Hilson Akana Kufanya Upasuaji wa Kurekebisha Pua

MWANAMUZIKI wa Marekani Keri Hilson amemjibu kwa jazba shabiki mmoja ambaye alidai kuwa msanii huyo amefanya upasuaji wa kuweka pua yake kwenye muonekano murua zaidi.

Shabiki huyo alitoa kauli hiyo kwenye picha aliyoweka Keri Hilson kwenye ukurasa wake wa instagram ambapo aliweka picha ikimuonyesha yupo na familia yake na Keri alikuwa bado mtoto, ndipo shabiki huyo aliandika “upasuaji wa pua uliofanya ni mzuri.”

Keri Hilson alimjibu kwa kusema kuwa hajawai kufanya upasuaji wowote kwenye mwili wake na watu wake wa karibu wanalitambua hilo.

Mara kwa mara watu wamekuwa wakisema kuwa Keri Hilson amefanya upasuaji wa kuweka pua yake kwenye muonekano mzuri jambo ambalo yeye mwenyewe amekuwa akilipinga vikali.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey