Kings Music ya Alikiba Yasambaratika
WASANII Killy na Cheed waliokuwa chini ya lebo ya Kings Music ambayo inamilikiwa na msanii nguli Alikiba wametangaza kujitoa rasmi kwenye lebo hiyo.
Wasanii hao kwa pamoja wametumia ukurasa wa instagram kutoa taarifa hiyo na wameyasema hayo alfajiri ya leo ya tarehe 14 Aprili 2020 na sababu walizotoa ni kuendeleza muziki wao binafsi.
Nyota hao kwa pamoja wameandika ujumbe uliofanana kwa kila kitu na kufanya mashabiki kuhisi kuwa ni wazo walilopanga kufanya kwa pamoja.
Hata hivyo Alikiba bado hajasema lolote kuhusu maamuzi ya wasanii hao kutoka kwenye lebo yake.
Toa Maoni Yako Hapa