Sambaza

Viatu vya Kanye West (Yeezy) Vyasababisha Vifo Viwili

Picha ya binti aliyeuawa

WAPENZI wawili wenye umri wa miaka 18 na 19 wameuawa kwenye dili la kuuza viatu aina ya Adidas Yeezy ambavyo ni bidhaa za msanii Kanye West.

Ripoti ya polisi imeeleza kuwa wapenzi hao walitafutwa na vijana wawili na kuomba kuuziwa viatu hivyo na kuwaambia mahali pa kukutania kisha marehemu hao walienda.

Katika eneo la tukio mmoja wa vijana waliokuwa wakinunua viatu aliomba kuvijaribu na ndipo mmoja akatokea kwa nyuma na kuwapiga risasi wote wawili na kuwauwa palepale.

Hata hivyo, vijana hao wamekamatwa na polisi na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kuua.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey