Sambaza

Diva, Alikiba Picha la Kihindi ‘Haliishi Leo’

Hakuna aliyewahi kutegemea kama mwanadada Diva na msanii Alikiba wanaweza kufikia hatua ya kuwa maadui kwa namna yoyote ile. Wawili hao wamekuwa marafiki kwa muda mrefu na mashabiki wa muziki waliona kama Diva ni mfuasi wa Alikiba ambaye hata ije mvua au jua bado atasimama naye.

Tamthilia ya Diva na Alikiba ndiyo kama imeanza na kionjo cha tamthilia hii kilirushwa hewani alfajiri ya jana tarehe 14 Aprili na wale waliokuwa wasanii wa Alikiba Killy na Cheed baada ya kuweka wazi kuwa wamejiondoa kwenye lebo ya msanii huyo.

Wengi walidhani ni njama za mjini ili kuupaisha muziki mpya wa Alikiba uitwao Dodo lakini kumbe ilikuwa ni kionjo tu cha tamthilia ambayo huenda ikachuka muda mrefu kuisha kama tamthilia za kihindi.

Basi bwana tamthilia yenyewe hatimaye imeruka hewani na inaongozwa na mwanadada mrembo maarufu kama Diva the Bawse ambapo ametumia ukurasa wake wa instagram kuhakikisha tamthilia hii inawafikia watazamaji wengi iwezekanavyo. Ameanza kwa kuweka picha ya Alikiba na kuandika ujumbe mrefu ambapo alidokeza kuwa alikuwa kwenye mahusiano na Alikiba kwa muda mrefu pia amedokeza kuwa anafahamu mipango ya Killy na Cheed baada ya kutoka Kings Music.

Wengi walidhani kwa mara ya kwanza tamthilia ya kihindi imekuwa tamu na fupi lakini kabla watazamaji hawajatoka kwenye banda la video mara kipande cha pili kikarushwa hewani na muongozaji yule yule Diva the Bawse baada ya kuweka mazungumzo ya maandishi baina yake na Alikiba hadharani. Watu wakarudi wakaketi kutazama kipande hichi cha pili ambacho kilionyesha dhahiri kuwa Alikiba na Diva walikuwa ni wapenzi.

Wengi wanasubiri kuona namna filamu hii itavyokuwa, je itakuwa ndefu na tamu kama filamu za kihindi? Ama itakuwa fupi na tamu kama filamu za ucheshi wa Joti?

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey