Sambaza

Kanye West Azungumzia Kuokoka, Kumpigia Trump Kura, Muziki wa Injili

Kwa muda mrefu Kanye West hajashika vichwa vya habari hasa kwa kauli na maamuzi yake tata ila sasa kusubiri kumekwisha. Kanye amefanya mahojiano na jarida moja nchini Marekani na kuzungumzia mambo kadhaa.

Kumpigia Kura Trump:

Kanye West amesema kuwa uchaguzi wa mwaka huu atapiga kura na inafahamika ni nani atakayempigia kura sio mwingine bali Rais Donald Trump.

Kuhusu Kufanya Muziki wa Injili:

Kanye West alisema “nilikuwa nawaza kuacha kurap sababu nimemuimbia shetani kwa muda mrefu kiasi kwamba sikujuwa ata namna ya kumuimbia Mungu. Siku moja mchungaji wangu aliniambia ‘mtoto wangu aliniambia anatamani kusikia album ya rap kutoka kwa Kanye West’ na hilo neno moja liliweka tofauti kwangu.”

Kuacha Vilevi:

“Nilikuwa nafanya kazi ofisini kwangu siku moja na nikasema ngoja nikapate kinywaji kimoja cha mchana ila nikasita nikasema nimekuwa nikitumia vilevi tangu nilipojua kuwa nataka kutumia basi leo shetani hutoniweza, na hivyo ndivyo nilivyoacha.” Alisema Kanye West.

Kutumia Iphone Kurekodi nyimbo:

Nyota huyo alijibu kuwa “huwa ninarap kwenye simu yangu kila muda mfano album ya Jesus Is King kuna nyimbo mbili ambazo ni ‘Chic Fil’ A’ na ‘Closed on Sunday’ nilizirekodi kwenye simu, iphone ina maiki nzuri.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey