Sambaza

Snoop Dogg Amkaripia Bill Gates Kama Mtoto Mdogo

Rapa Snoop Dogg ni miongoni mwa maelfu ya raia wa Marekani ambao wapo majumbani mwao kupisha janga la Corona na Snoop ametumia muda huo kucheza michezo ya runinga (video games) ili asiwe mpweke na michezo anayopendelea kucheza ni ile iliyotengenezwa na kampuni ya EA Sports ambayo inamilikiwa na tajiri Bill Gates.

Katika hali ambayo ni nadra kutokea, mchezo huo ulipata hitilafu na kupelekea kutofanya kazi kwa muda na hapo ndipo msanii huyo alipowaka na kuwakaripia wahusika kwa kutumia video fupi aliyoweka kwenye ukurasa wake wa instagram.

“EA Sports, mtandao wenu haufanyi kazi, tunataka kucheza, tumefungiwa majumbani, tengenezeni hili haraka, Bill gates, Microsoft yeyote yule fanyeni kutengeneza, sasa hivi.” Alisema nyota huyo ambapo aliambatanisha na majina ya Bill gates na Microsoft.

Hata hivyo baada ya muda mfupi Snoop Dogg aliweka video nyingine ambayo aliwashukuru kwa kumpa taarifa kuwa itarudi muda sio mrefu kisha akamalizia kwa kusema “mnaweza kurudi kwenye ratiba zenu kama kawaida sasa.”

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey