YNW Melly Hatoruhusiwa Kutoka Jela Japo Anaumwa Corona
Ombi la msanii wa Marekani YNW Melly ambaye anakabiliwa na mashtaka mawili ya jinai la kuomba kutolewa jela ili kuwa karibu na huduma za afya limekataliwa na mahakama.
Wiki kadhaa zilizopita, wakili wa msanii huyo alisema kuwa mteja wake amepata maambukizi ya ugonjwa wa Corona akiwa magereza hivyo sio sehemu salama kwake na akaahidi kuiomba mahakama ili wamtoe msanii huyo angalau kwa dhamana akapate matibabu.
Melly amekuwa akisumbuliwa na dalili za ugonjwa huo kama homa kali, kupumua kwa shida, maumivu ya mwili na maumivu ya kichwa ila hayo yote hayajaweza kuishawishi mahakama kumpatia dhamana nyota huyo.
“Kama Melly anataka kupata matibabu ndani ya gereza anapaswa kuzungumza na mkuu wa gereza ili apatiwe matibabu hayo” alisema hakimu wa mahakama hiyo.