50 Cent Muuza Pombe Asiyetumia Kilevi
50 Cent ameamua kusimamia msimamo wake wa kutotumia kilevi chochote japo ni mmiliki wa kampuni mbili za kutengeneza pombe.
Kwenye kitabu chake cha “Hustle Harder, Hustle Smarter” ameelezea ni namna gani ameweza kuwa safi bila kutumia kilevi japo ni muuzaji wa pombe.
“Kwa kawaida nitachukua chupa moja ya pombe kisha nitawamiminia rafiki zangu wote halafu pombe ikiisha nitamuita kijana wangu mmoja na kumwambia akanijazie kinywaji chepesi kisicho na kilevi na usiku mzima nitatumia hicho,” alisema msanii huyo.
50 Cent ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye utayarishaji wa filamu alisema anakumbuka siku ambayo alikutana na Snoop Dogg na akamwambia avute japo pafu moja ya bangi na ikambidi avute japo aliuvuta moshi ule na kuucha mdomoni bila kuupeleka popote na kuutoa, kisha akamalizia kwa kusema, “Bill Clinton amevuta moshi mwingi wa bangi zaidi yangu.”
Mapema wiki hii msanii huyo alikataa ombi la hasimu wake wa siku nyingi, Ja Rule, la kupambanishwa naye kwenye ukurasa wa instagram.
Kitabu cha “Hustle Harder, Hustle Smarter” kitatoka tarehe 28 Aprili 2020.