Cardi B Azungumza Mambo ‘Siriaz’ Kwa Mara ya Kwanza
Wapenzi wa muziki na hata mashabiki wake wanatambua kuwa Cardi B ni mtu wa vituko na kuzungumza utani mara zote ila huenda mtazamo huo ukaisha baada ya Cardi B kuzungumza na kiongozi wa kisiasa Bernie Sanders.
Mazungumzo hayo yamefanyika kupitia “instagram live” ya Cardi B ambapo alianza mwenyewe kisha akamualika kiongozi huyo wa Democratic ambaye alikuwa anagombea kupata tiketi ya kugombea urais kutoka kwenye chama chake.
Baada ya kusalimiana, mwanadada huyo alianza kuongoea kwa hisia na kusema “nimeumia na kukasirika kwa maamuzi yako ya kujitoa kwenye mbio za kugombea urais” alisema “nilikasirika kwa sababu nilikuwa nikiwaambia vijana na mashabiki wangu kuwa tunapaswa kukupigia kura, sasa tumebaki na chaguo mbili tu Joe Biden na Trump.”aliongeza Cardi B.
“Nimeamua kumpigia kura Joe Biden japo sijafanya tafiti kuhusu yeye lakini naamini ni mtu mzuri na pia nimefurahi kuona Barack Obama anamuunga mkono,” alisema msanii huyo.
Hata hivyo Bernie Sander alisema kuwa alipanga kumuunga mkono kiongozi yeyote yule atakayepewa nafasi na chama cha Democratic ili tu wamtoe Rais Donald Trump madarakani na kumuita “Rais hatari zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya Marekani.”