Sambaza

Ja Rule, 50 Cent Jino kwa Jino Mpaka kieleweke

HUENDA Corona isiishie kutawanya mataifa peke yake bali kufufua na ‘bifu’ za miaka ya nyuma.

Siku kadhaa zilizopita Ja Rule ambaye ni hasimu wa 50 Cent kwa muda mrefu alifanya mahojiano na kuweka wazi kuwa yupo tayari kushindanishwa na 50 Cent kwenye mashindano  yanayoendelea kwenye mtandao wa instagram.

50 Cent alijibu kwa kuweka picha mbili kwenye ukurasa wake ambazo zinamkejeli Ja Rule nakuambatanisha ujumbe kuwa Ja Rule anataka kushindana naye ili apate ‘kiki.’

Imemchukua siku kadhaa kwa Ja Rule kujibu mashambulizi na hatimaye naye ameweka picha kwenye ukurasa wake wa instagram, picha ambayo imamuonyesha 50 Cent kama mwenye masikio, pua na meno ya sungura kisha akaandika “Ohh unataka vikatuni, Curtis Ratson yupo mpweke nyumbani na mimi nipo nyumbani mpweke.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey