Nai Akiri Kuachana na Moni Centrozone
VIDEO vixen Bongo, Nai amekiri kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Moni Centrozone huku akiwataka watu waendelee kuongea, lakini hawezi kumrudia ng’o.
Akibonga na Amani, Nai alisema kuwa kuachana ni kawaida na mara kwa mara watu wamekuwa wakitabiri kuwa wataachana na sasa wameachana kweli.”Kwa sasa tumeachana kweli na siwezi kurudiana na Moni japokuwa tumetoka mbali tangu tukiwa Dodoma.
Kuachana ni kawaida, wanaachana watu wakiwa wamezaa watoto nane, itakuwa sisi hata mdoli hatuna? Kuhusu kuondoka na vitu siyo kama watu wanavyosema,” alisema Nai
Toa Maoni Yako Hapa