Nicki Minaj Afunguka Kuhusu Album, Kuanzisha Lebo, Ugomvi na Meneja
Nicki Minaj ambaye amepotea kabisa kwenye mitandao ya jamii hivi karibuni, ameibukia kwenye mahojiano aliyofanya na meneja wake wa kwanza kwenye maisha yake ya muziki.
Wawili hao walikuwa na ugomvi kwa zaidi ya mika 10 ambapo walizungumzia hilo kwa meneja huyo kusema “Sikufurahi kuona sifa zote anapewa Lil Wayne wakati kiuhalisia mimi ndiye wa kwanza kugundua kipaji chako.”
Nicki alijibu kwa kusema “naelewa huenda ulidhani sijakupa heshima yako ila kiukweli unastahili na nakuheshimu sana sababu uliwekeza pesa, muda, nguvu kuhakikisha nafika hapa nilipo leo.”
Pia rapa huyo alizungumzia ujio wa album yake ambayo alisema kuwa amekuwa akijitafuta ili awape mashabiki ladha tamu. Anasema “ilinichukuwa dakika tu kujipata lakini sasa nahisi natakiwa kujitafuta tena ili nisiwaangushe shabiki zangu.”
Mbali na hayo yote pia msanii huyo ametoa habari nzuri kwa wasanii wadogo kwani amesema anatarajia kuanzisha lebo yake na amekuwa akitafuta kipaji cha kukisajili. Nicki alikazia kwa kusema “rapa wa kike au wa kiume, muimbaji wa kike au wa kiume yeyote tu sijali.”