Breaking: Kifo cha Mama Rwakatare, Shigongo Aeleza Mazito – Video
MCHUNGAJI wa Kanisa la Mlima wa Moto, Askofu Gertrude Rwakatare, amefariki dunia alfajiri ya leo ya Aprili 20, 2020, akiwa na umri wa miaka 69.
Taarifa iliyotolewa na mwanaye, Muta Rwakatare inasema: “Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo. Jana tulimkimbiza hospitali lakini bahati mbaya imetokea. Tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu.”
Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizokuwa nazo kabla ya kukutwa na umauti, alikuwa alikuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Dkt. Rwakatare alizaliwa Disemba 31, 1950.
Toa Maoni Yako Hapa