Blac Chyna, Rob Kardashian Kwenye Vita ya Kisheria Isiyoisha
Kumekuwa na mapambano ya kisheria baina ya Blac Chyna na Rob Kardashian kwa muda mrefu. Wawili hao walikuwa wapenzi na wana mtoto mmoja ambaye amekuwa chanzo kikubwa cha wawili hao kufikishana mahakamani mara kwa mara.
Mwezi uliopita Blac Chyna alilalamika kuwa mwanao huyo alipata majeraha kadhaa akiwa nyumbani kwa baba yake Rob. Wakili wa mrembo huyo alisema kuwa Rob alikiri kosa na kuapa kutotokea tena.
Rob Kardashian, huenda ameamua kulipiza kisasi baada ya kufungua kesi kuwa mrembo Blac Chyna alimshikia silaha. Japo mwanadada huyo amejitetea kuwa alikuwa akifanya utani ila timu nzima ya wanasheria wa Rob wanasema kuwa tukio hilo lilishuhudiwa na watu kadhaa.
“Blac Chyna hafanyi jitihada zozote kuhusu mashahidi hao sababu anajuwa ni ukweli tunachosema,” alisema wakili wa Rob Kardashian.