Sambaza

Drake Aongeza Umaarufu wa Kundi la Kucheza Muziki Kutoka Africa

Wimbo mpya wa Drake “Toosie Slide” unafanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii na ameanzisha shindano la kucheza wimbo huo ambalo pia limekuwa na muitikio mkubwa.

Kundi la kucheza muziki kutoka Uganda linalofahamika kwa jina la “Masaka Kids Africa” limekuwa miongoni mwa walioshiriki shindano hilo na Drake mwenyewe ametia neno na kufanya kundi hilo kupata mashabiki wapya na umaarufu kukua.

Akifanya mahojiano na TMZ, Suuna Hassan ambaye ndiye mvumbuzi wa kundi hilo alisema “watoto wale walitaka kushiriki kwenye shindano hilo sababu wanaupenda wimbo huo na walikuwa wakiomba Drake aweze kuwaona japo lilikuwa ni jaribio gumu.”

Kitu kilichowavutia wengi ni Drake alipoamua kuwatumia ujumbe mfupi wa kuwaomba wamtumie video hiyo na walimtumia ndipo Drake akaiweka kwenye ukurasa wake.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey