Sambaza

French Montana Afunguka Bifu na 50 Cent, Kutotumia Kilevi, kula sumu akiwa Africa

Rapa French Montana amekuwa ni msiri wa mambo yake lakini amefunguka kiasi cha kutosha kwenye mahojiano aliyofanya na 99 Jamz.

“Leo nafikisha mwezi wa tano sijatumia kilevi” alisema Montana na kuongeza “nataka nione nitafanya hivyo kwa muda gani, nimekuwa kwenye tasnia tangu 2002 na sasa naona huu ndio wakati wa kubadilika, siwezi kutengeneza milioni 100 kama nimelewa.”

Akizungumzia suala la afya yake ambayo ilikuwa mashakani wakati uliopita amesema ni kutokana na kula chakula chenye sumu alipokuwa Africa. Pia amesema “mbali na hiyo (sumu) pia nina jishughulisha sana ndiyo maana wakati mwingine napata matatizo ya kiafya.”

Alipoulizwa kuhusu bifu na 50 Cent alijibu “najaribu kumtafuta tufanye kazi, sidhani kama kuna bifu, nachoona ni utamaduni wa hip hop tu watu wanajaribu kutushindanisha ila sio bifu.”

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey