Sambaza

J Lo na Mumewe Wapo ‘Siriazi’ Kuinunua Timu

Kumekuwa na stori za chini chini kuhusu J Lo na mumwe Alex Rodriguez kutaka kununua timu ya besiboli ya NY Mets na sasa stori hizo zinageuka kuwa ukweli baada ya wawili hao kuonyesha nia ya kufanya hivyo.
Imeripotiwa kuwa wamemtafuta JPMorgan Chase ili aweze kufanya namna ya kutafuta pesa ili waweze kununua timu hiyo.
Wengi watajiuliza kwa nini matajiri kama wao watafute pesa ili kununua timu, kwani hawana pesa?


Timu hiyo sio ya bei rahisi kwani tayari wapo watu kadhaa waliowai kutoa dau zao ikiwemo dau la Dola za Marekani 2.6 Bilioni ambalo nalo lilikataliwa.
Familia ya Wilpon ambao ndiyo wamiliki kwa sasa wa timu hiyo wapo tayari kuiuza kwa yeyote atakayefika dau.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey