Sambaza

Jose Chameleone Ageukia Muziki wa Injili

Nguli wa muziki Africa Jose Chameleone amefanya tena wimbo wa injili ambao unaitwa “Bolingo ya Nzambe” ambapo ni wimbo wa kwaya ya kilutheri aliyokuwa akiimba alipokuwa mtoto.

Jose Chameleone ameandika “nilipokuwa mtoto nilikuwa mmoja wa wana kwaya wa “Holy Family Catholic Church Kawempe” na huu ndio uliokuwa wimbo nilioupenda zaidi. Miaka kadhaa mbele, siku ya harusi yangu mke wangu aliuchagua wimbo huu (bila mimi kujua) sababu alijuwa namna navyoupenda, kwa kweli nilihisi mbingu zimeshuka na sitasahau siku hiyo.”

“Hivi karibuni nilitamani kuusikia tena na nikautafuta ila sikuupata, kwa kipaji alichonipa Mungu nimetengeneza wimbo huo tena na ninatumaini mtaufurahia,” aliongeza Jose Chameleone.

Hii ni mara ya pili kwa msanii huyo kutoa wimbo wa injili baada ya Tubonge aliotoa mwaka 2014.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey