Sambaza

Selena Gomez Awasweka Mahakamani Mabosi, Ataka Alipwe Bilioni 23

Wanasheria wa mwanadada Selena Gomez wamefungua shtaka kuwashtaki watengenezaji wa “gemu” la mtandaoni kwa madai kuwa mmoja wa vikatuni vya gemu hilo anafanana na Selena Gomez.

“Selena Gomez kupitia kazi zake za mitindo, muziki na uigizaji zimefanya jina lake kuwa chapa,” alisema mmoja wa mawakili wa mwanadada huyo. “Forgame, Mutanbox na Fly by Night ni magemu ambayo yametumia muonekano wa Selena bila ridhaa yake kitu ambacho ni kinyume cha sheria” aliongeza wakili huyo.

Kesi hiyo ambayo imejikita kwenye kusimamia haki ya kuwekwa hadharani ambapo Selena anasema alishangaa kuona muonekano wake umetumika na hakuna aliyeomba au kumjulisha kuwa itakuwa hivyo.

Endapo mrembo huyo atashinda kesi, itawalazimu watengenezaji wa magemu hayo kumlipa fidia Selena kiasi cha Dola za Marekani Milioni 10 (Bilioni 23 za Tanzania).

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey