Sambaza

The Weekend Aendeleza Ubabe, Amshusha Drake

Album inayofanya vizuri zaidi kwa muda huu ni album ya The Weekend iitwayo “After Hours” ambapo ndiyo namba moja kwa mwezi mzima.

Huenda huu ukawa mwaka mzuri kwake kwani licha ya album kwa ujumla kuendelea kufanya vizuri pia wimbo mmoja mmoja kutoka kwenye album hiyo zinaendelea kufanya vizuri.

Wimbo wa “Blinding Lights” umeshika namba moja kwenye chati za Billboard na kuushusha wimbo wa Drake “Toosie Slide.”

The Weekend hakusita kuonyesha furaha yake baada ya kuweka taarifa hizo kwenye ukurasa wa instagram na kuandika “wow nimerudi juu + album namba moja kwa mwezi mzima? Nitasherehekea huu wakati.”

Hii ni mara ya kwanza kwa msanii kuwa na albuminayoshika namba moja kwa mwezimzima tangu mara ya mwisho alipofanya hivyo Drake na album yake ya Scorpion.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey