Victoria Beckham Awachukiza Wafanyakazi, Awafyeka Mshahara
Victoria Beckham ambaye ni mke wa mchezaji maarufu David Beckham ameshika vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kuwa amewakata wafanyakazi 30 mishahara kwa 20%.
Wafanyakazi hao walipokea barua kuwapa taarifa kuwa watakatwa asilimia 20 ya mishahara yao. Msemaji wa mrembo huyo amedhibitisha kuwa zoezi hilo itafanyika hivyo kwa miezi 2.
Piers Morgan ambaye ni mchochezi wa watu kupigania haki zao ametoa taarifa hiyo na kusema kuwa mwanadada huyo ni milionea anayetaka kupewa upendeleo anayetaka kutumia ushuru kama kisingizio cha kuokoa biashara inayokufa.
Kwenye mitandao ya kijamii, wengi wamekasirishwa na hatua zilizochukuliwa na Victoria Beckham hasa ukizingatia kuwa inaaminika kuwa mwanadada huyo na mumewe wamenunua mjengo wa mabilioni ya pesa wiki mbili zilizopita.