Sambaza

Davido Apewa Shavu na Khalid

Msani wa Nigeria Davido anaendelea kupasua anga na kucha viza kwa kolabo za kimataifa ambapo sasa ameshirikishwa kwenye wimbo mpya wa msanii wa Marekani Khalid.

Khalid ambaye ametamba sana na vibao mbali mbali ikiwemo “location” wimbo ambao ulimuingiza kwenye tuzo za MTV amethibitisha kuwa wimbo unaotoka tarehe 23 Aprili amemshirikisha Davido na mwanadada toka Nigeria Tems.

Kupitia twitter Khalid alieka kionjo cha wimbo wao huo ambapo aliandika “Know Your Worth remix pamoja na Davido na Tems itatoka 23/4 nasubiri kwa hamu.”

Imekuwa ni kawaida kwa wasanii wa Nigeria kupata mashavu kutoka kwa wasanii wakubwa wan je ya Africa ambapo Tems naye anaungana na Tekno, Tiwa Savage, Davido, Wizkid, Rema na wengine wengi kwenye wasanii wenye kolabo kubwa za nje ya Africa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey