Ibraah: Sina Nyimbo na Harmonize, Sijui cha Kumlipa
MSANII aliyetambulishwa na lebo ya Konde Gang siku za karibuni Ibraah amefunguka kuwa mpaka sasa bado hajafanya kazi na Harmonize.
Akichezesha taya na Isri Mohammed wa Global Tv Online, msanii huyo alijibu swali la shabiki aliyeuliza kama tayari amefanya kazi nakonde boy na akajibu “nyimbo na konde boy bado sijafanya naye.”
Hata hivyo hakusita kuweka wazi matamanio yake ya kufanya kazi na msanii huyo wa kimataifa ambapo alisema “kutamani lazima nitamani kufanya naye maana ni sanii anayesikilizwa dunia nzima, naomba Mungu siku ifike niweze kupata bahati ya kufanya naye kazi.”
Mbali na hayo msanii Ibraah aliulizwa na shabiki wake ni nini atamfanyia Harmonize kama fadhila naye akajibu “kwa kweli sijui cha kumlipa ila Mungu atakavyozidi kunibariki vipo ambavyo nitafanya Watanzania wenyewe wataona.”