Sambaza

Young Thug Amuwashia Moto French Montana

Ugomvi wa Young Thug na French Montana haujawaka tu bila kibiriti, La! Bali ni maneno ya French Montana ndiyo yaliyopelekea Young Thug kumjia juu kwa kejeli na matusi kibwena.

French Montana alisema “Nina uwezo wa kushindana na yeyote, watu hawajui nipo kwenye muziki kwa miaka takribani 20, ninaweza kuwekwa kwenye tamasha na Kendrick Lamar lakini nikamfunika, sio kwa sababu mimi ni rapa mkali kuliko yeye ila ni kwa sababu nyimbo zangu ni maarufu zaidi.”

Young Thug aliweka video fupi kwenye ukurasa wake ikimuonyesha akisema “huyu jamaa anasema ana nyimbo nyingi maarufu kuliko Kendrick?” kisha akacheka.

Baadaye Young Thug aliweka tena video nyingine ambapo hii ilkuwa ndefu kidogo huku akimkejeli French Montana na kumtusi pia.

Hata hivyo video hizo zilifutwa na Young Thug.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey