Sambaza

Madee Hataki Tena Kusherehekea ‘Birthday’

Nguli wa muziki wa kufoka Tanzania Amadi Ally a.k.a Madee amewaza na kuwazua na kuona hakuna haja ya kusherehekea siku ya kuzaliwa zaidi ya kuhuzunika.

Msanii huyo ambaye leo tarehe 23 Aprili ndiyo siku yake ya kuzaliwa ameandika kwenye ukurasa wake wa instagram kwa kusema kuwa ameanza kupata ukakasi kusherehekea siku ya kuzaliwa  kwa sababu anachoamini ni umri unaposogea ndivyo kifo kinavyo karibia.

Hata hivyo ameweka bayana kuwa pesa ya kufanya sherehe hiyo ameamua kuielekeza kusaidia familia zenye uhitaji mtaa wa Manzese Jijini Dar Es Salaam kwa kuizpatia vifaa kinga dhidi y Corona.

Je unakubaliana na mawazo ya Madee?

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey