Sambaza

Mama wa Juice WRLD Amuenzi Mwanaye

MAMA wa marehemu Juice WRLD aitwaye Carmel Wallace ametangaza kuanzisha mfuko maalumu uitwao “Live Free 999 Fund” kusaidia vijana ikiwa ni njia ya kuenzi mema ya mwanaye.

Hii imekuja miezi kadhaa toka msanii huyo afariki kwa kuzidisha madawa ya kulevya.

Mfuko huo utapewa nguvu na Interscope Records na Grade A (makampuni ya muziki yaliyokuwa yakifanya kazi na Juice WRLD) na utaanzisha kampeni mbali mbali za kusaidia vijana wenye matatizo ya uteja, wasiwasi na msongo wa mawazo hasa kwenye jamii yenye asilimia kubwa ya matatizo hayo.

“Vijana wengi waliguswa na muziki wa Jarad (Juice WRLD) kwa sababu aliongelea matatizo yanayowagusa moja kwa moja” Alisema mama huyo.

“Nilifahamu kuhusu aliyokuwa akipitia na nilizungumza naye mara kwa mara, najuwa alikuwa anatamani kuwa huru na utumwa huo, nilifanya maamuzi baada ya kifo chake kuwa nitashirikisha dunia juu ya mapambano ya mwanangu.” Aliongeza mama yake Juice WRLD.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey