‘The New Toronto 3’ Album ya Tatu Kwa Tory Lanez Kufika Namba 1 Billboard
HUENDA kwa sasa Tory Lanez atakuwa nyumbani kwake ili kujikinga na Corona lakini kwa hakika atakuwa anagonga ‘cheers’ na rafiki zake baada ya kuweka historia na album yake mpya.
Kwa mujibu wa Billboard, Album hiyo imetazamwa mara 64,000 na kama unashangazwa na mafanikio hayo ya Tory Lanez basi haupo peke yako kwani hata yeye ameonyesha kushangzawa.
Rapa huyo alisema “sijui hata imefanikiwaje, sikuifanyia matangazo nilidhani itauza kama 10,000.”
Rapa huyo aliwahi kusema kuwa anaamini atakuja kuwa msanii mkubwa duniani na huenda yupo njiani kufanikisha hilo.
Toa Maoni Yako Hapa