Sambaza

Licha ya Kifungo Huru, Takeshi 69 Aomba Kufanya Video

Msanii mwenye vituko kibao Takeshi 69 anaendelea na kifungo cha nje ambapo anavaa bangili maalumu mkononi ili kuhakikisha mahakama inamuona kila anapokwenda ili asitoke nje ya mipaka aliyo wekewa.

Aprili 2 mwaka huu msanii huyo aliruhusuiwa kumalizia kifungo chake  nje ya magereza sababu ana ugonjwa wa Asthma na janga la Corona lingehatarisha maisha yake zaidi endapo angeendelea kukaa ndani.

Hata hivyo aliruhusiwa kuendelea na shughuli zake za muziki na pia kutumia mitandao ya kijamii japokuwa huenda hajaridhika na ameomba aruhusiwe kufanya na video za nyimbo zake na amesisitiza kuwa atafanyia nyuma ya nyumba yake.

Tutaendelea kukujuza majibu ya mahakama endapo ataruhusiwa au la!

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey