Sambaza

Lil Wayne Kutuletea ‘Young Money Radio’

HABARI nzuri kwa mashabiki wa Lil Wayne ambao wamekuwa na kiu ya angalau kusikia wimbo mpya kutoka kwake, sasa ameleta hii japo sio  wimbo ila ni wazi kuwa mashabiki wake wataipenda.

Rapa huyo alitumia ukurasa wake wa twitter kutupasha habari kuwa anaanzisha “Young Money Radio” ambayo atakuwa akihoji watu maarufu mbalimbali kujadili maisha na kazi zao.

Pia Lil Wayne alisema kuwa kipindi hicho kitakuwa kinarushwa kwenye “instagram live” kwa muda mchache kisha kipindi kitaendelea kwenye “Apple Music” ambalo ni jukwaa la kuuza na kusambaza muziki.

Apple Music ambao hivi karibuni walitangaza kuingia rasmi Tanzania ndio watakaohakikisha burudani hii inakufikia kiganjani mwako ambapo itaanza rasmi leo tarehe 24 Aprili.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey