Kanye West Aingia Rasmi Kwenye Ubilionea
BENKI ya nguli wa muziki wa kufoka, prodyuza na mwanamitindo, Kanye West, imefikisha tarakimu tisa rasmi, yaani kuna bilioni na zaidi kwa mujibu wa Forbes.
“Kwa takwimu zetu za kuaminika, bidhaa za viatu aina ya Yeezy vimesababisha Kanye West kufikisha utajiri wa dola za Marekani bilioni moja na zaidi kidogo,” walisema Forbes ambao wanaaminika kwa kufanya takwimu za utajiri.
Pia wameweka wazi kuwa nyaraka zinazoonyesha utajiri wa msanii huyo vilevile zinaonyesha kuwa viatu vya Yeezy viliingiza jumla ya mapato ya dola za Marekani bilioni 1.9 ambapo mkataba wake na kampuni ya Nike unamfanya msanii huyo kuchukua 15% ya mapato ya viatu hivyo.
Sasa Kanye West anaungana na Jay Z, Oprah, Floyd Mayweather na wengine miongoni mwa watu maarufu wanaomiliki mkwanja mrefu.