Sambaza

Kodak Black Aomba Kukutana na Rais Trump, Amruhusu Kumuua

Msanii Kodak Black amewashtua wengi baada ya kutuma ujumbe wa kumuomba Rais Donald Trump aende kuonana naye jela ambapo msanii huyo amefungwa.

“Mwambie Trump aje anione nina wazo zuri” alisema Kodak na kuendelea “siku za nyuma nilipata wazo lakini nikalipotezea sababu sikuona kama ni muhimu sana muda huo, lakini hili wazo limekuwa likinifata japo sina cha kufanya sababu ya kifungo changu cha makosa, njoo tuonane nimevaa barakoa.”

Kwa kuonyesha msisitizo msanii huyo aliongeza kwa kusema “kama wazo hilo halina maana kwa namna yoyote unaweza kuniua.”

Nyota huyo ambaye anatumikia kifungo ambacho kinatarajiwa kuisha Oktoba 2022, hali hiyo haijamfanya Kodak asiendelee kushika vichwa vya habari mbali mbali.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey