Sambaza

Mike Tyson: Floyd Mayweather Atakuwa Kocha Mzuri

SIKU za karibuni Floyd Mayweather alisema kuwa njozi zake ni kutumia ujuzi na uzoefu alionao kwenye mchezo huo kufundisha kizazi kijacho na TMZ wakaamua kuuliza mawazo ya nguli wa mchezo huo, Mike Tyson, juu ya kauli ya Mayweather.

Tyson amesema kuwa kama Mayweather anataka kuwa kocha wa ngumi atakuwa kocha mzuri.

Nguli huyo wa masumbwi aliongelea tofauti kati ya  Mayweather na mabondia wengine na alisema anatambua kuwa wengi wa makocha wa masumbwi huwa si mabondia wazuri ila Floyd yupo tofauti.

“Ninampa Floyd nafasi kubwa ya kuwa kocha mzuri sababu ni chizi wa mazoezi,” alisema Tyson na kuongeza,  “muda wote yupo chumba cha mazoezi, unaweza kumuona kwenye starehe kwa wiki moja lakini yupo kwenye chumba cha mazoezi kwa miaka 25.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey