Sambaza

‘Circles’ ya Post Malone Yavunja Rekodi

POST MALONE amevunja rekodi yake mwenyewe baada ya wimbo wake wa Circles kufikisha wiki 34 ndani ya orodha ya nyimbo 10 za juu kwenye chati za Billboard.

Wimbo huo ambao ulishika namba moja kwa wiki tatu, umeendelea kufanya vizuri kwenye chati hizo baada ya kupiga hatua moja mbele kutoka namba 7 hadi 6.

Wimbo huo mpaka sasa umechezwa redioni mara bilioni 2.9 na umesikilizwa mtandaoni mara milioni 732 (Marekani tu) pia umepakuliwa zaidi ya mara laki 4.

“Huu ni wimbo ambao kila nikiusikiliza ninafurahia kama kwamba ndiyo mara ya tatu au nne nausikia,” alisema mtaalam mmoja wa muziki.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey