Ed Sheeran Akataa Pesa za Serikali Kuwalipa Wafanyakazi wa Baa Yake
Msanii Ed Sheeran amekataa kuchukua pesa za serikali ili awalipe wafanyakazi wake kufuatia kufungwa kwa baa yake iliyopo kwenye jiji la London kutokana na janga la Corona.
Kwa mujibu wa Daily Mail mwanamuziki huyo amekataa kupokea asilimia 80 ya mshahara wa wafanyakazi wake kutoka kwenye serikali ya Uingereza.
Habari hizi zimekuja wiki kadhaa mbele baada ya shutuma za Victoria Beckham kuiomba serikali kutomtoza kodi ili aweze kuwalipa wafanyakazi wake 30.
Msemaji wa Ed Sheeran amesema “Ed hayupo tayari wala hatochukua pesa za serikali iwe ni mkopo au la.”
Baa hiyo ilifunguliwa mwaka 2019 na inasemekana imepewa jina la mke wa Ed Sheeran Cherry Seaborn.
Toa Maoni Yako Hapa