Kid Cudi Ambadili Selena Gomez, Sasa ni Mwana Hip Hop
Ni ngumu kuwaza kuwa msanii wa Pop Selena Gomez ni shabiki wa muziki aina ya Hip hop sababu hajawai kuonyesha mahaba yoyote kwa muziki huo.
Kwenye album yake iliyopita alimshirikisha Kid Cudi ambapo toka hapo wamekuwa marafiki wazuri na Kid Cudi amekuwa akijaribu kumfanya mwanadada huyo aupende muziki wa Hip hop.
Selena Gomez ameweka wazi kuwa ni marafiki wazuri kwa sasa na wana wimbo wa pamoja ambao haujatoka na pia amesema namna Kid Cudi anafanya juhudi ili (Selena Gomez) aupende muziki wa kufoka.
“Yeye ndiye aliyenifanya niwasikilize kina Miss Elliott, Da Brat, Eve na wasanii wa kike wanaofoka,” alisema Selena Gomez
Toa Maoni Yako Hapa