Sambaza

Kodak Black Amuomba Nas ‘Kolabo,’ Amwita Mfalme

MSANII Kodak Black anatumikia kifungo lakini ni kama yupo huru tu. Amekuwa akiendelea na usumbufu kwenye mitandao ya kijamii. Mwanzoni mwa mwezi huu alirushiana maneno na NBA Youngboy na baadaye mwanzoni mwa wiki hii ameomba kuonana na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Sasa amegeukia kazi na amemtumia ujumbe nguli wa muziki wa kufoka Nas na kumuomba ‘kolabo’ hadharani.

Kodak alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika, “Salamu mfalme, nina wimbo ambao nakuhitaji, tafadhali ukipata nafasi naomba uusikilize na ikiwezekana uufanyie kazi.”

Je, Nas atakubali kufanya kazi na Kodak? Tutakujuza yote yatakayojiri.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey