Mama Mtoto wa Future Amzidi Kete Future Mahakamani
MWANADADA Eliza Reign ambaye alizaa na msanii Future amefungua kesi kudai pesa za matunzo ya mtoto.
Eliza amedai kuwa Future ni baba wa mtoto wao huyo lakini amekataa kutoa pesa za matunzo, Eliza akiamini kuwa anastahili kupata dola za Marekani 53,000 kwa ajili ya matunzo ya mtoto
Mapema mwezi huu Future alidai kuwa Eliza anatafuta umaarufu na kujaribu kujinufaisha kupitia jina la nyota huyo, lakini hakimu aliyafutilia mbali madai ya msanii huyo.
Kwa kufurahia ushindi huo mwanadada Eliza aliweka picha kwenye ukurasa wa instagram na kuandika “ukweli una nguvu kuliko uongo.”
Toa Maoni Yako Hapa