Sambaza

Brandy Kurudi Kwenye Tasnia na ‘Baby Mama’

Ni mara chache sana kuona Brandy akishika vichwa vya habari kwa sababu ni mtu wa kufanya vitu kimyakimya, ila hii imetufikia.

Mwanamuziki huyo ameweka tangazo fupi kwenye ukurasa wake wa twitter ikiwa inaonyesha kuwa kuna wimbo upo njiani na amemshirikisha Chance The Rapper.

Habari za kuaminika zinasema kuwa mwanadada huyo alikuwa amepanga kuachia wimbo huo Siku ya Mama Duniani.

Kumshirikisha Chance The Rapper ambaye amekuwa akitoa sifa kibao kwa mama watoto wake, ni jambo ambalo wengi wanaona itakuwa miongoni mwa “kolabo” nzuri.

Brandy ambaye hajatoa album tangu 2012, antarajiwa kufanya hivyo mwaka huu huku wimbo wa “Baby Mama” ukiongoza njia.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey