Gavana Aomba Radhi Kumtuhumu Kijana Aitwaye Shakur
JAMAA mmoja nchini Marekani ambaye anaitwa Shakur amejikuta akiingia matatani baada ya Gavana wa mji wa Kentucky kumtuhumu kutumia jina la “Tupac Shakur” kujipatia mafao.
Kijana huyo ambaye alipoteza kazi yake ya upishi na kujaza fomu ya watu wasio na ajira, kitu ambacho kilimfanya gavana huyo kudhani anafanya udanganyifu sababu ya jina lake kufanana na la Tupac.
Hata hivyo, ilimlazimu gavana kuomba msamaha baada ya kugundua kuwa alifanya makosa na alisema, “Niliongea na Shakur kwa njia ya simu.”
Aliongeza na kusema, “nilimwambia namna ilivyotokea na nikamwomba msamaha kwa kumuaibisha na ni kijana mzuri, tulimaliza maongezi yetu kwa yeye kusema ‘Mungu akujalie’.”
Toa Maoni Yako Hapa