Nadia Mukami: ‘Natamani Mungu Asingeniamini Kiasi Hiki’
MWANAMUZIKI kutoka Kenya, Nadia Mukami, ambaye anatamba na kibao chake alichomshirikisha Marioo wa Tanzania kinachoitwa “Jipe”, amesema ameachana na mitandao ya kijamii kwa muda.
Anasema idadi ya kejeli alizopata kwa miezi ya karibuni imemfanya kuumia moyo mara kwa mara.
“Naandika haya nikiwa natokwa machozi, najua wanasema mimi ni mtu maarufu sipaswi kuonyesha hisia ila nitaonyesha hisia, hakuna aina ya kejeli ambayo sijapewa,” alisema mwanamuziki huyo.
“Huu umekuwa mwezi wa kuumia moyo mara kwa mara, huwa Mungu hawezi kukupa kitu usichoweza kukibeba ila natamani asingeniamini kiasi hiki, ninapumzika nitarudi baadaye,” aliongeza.
Kejeli zilianza baada ya mama mmoja kuandika kwenye ukurasa wa facebook kuwa mwanamuziki huyo alimtapeli shilingi 15,000 za Kenya.