Sambaza

Harmonize Atangaza Tarehe Rasmi ya Kutoka Kwa EP ya Ibraah

TAREHE ya kuzindua EP ya msanii mpya wa Konde Gang Worldwide imewekwa bayana.

Kupitia Ukurasa wa Instagram msanii Harmonize ametoa taarifa hizo kwa kuandika “Steps The EP 8/05/2020”

EP hiyo ambayo tayari tulishadokezwa kuhusu orodha ya nyimbo zilizomo na baadhi ya wasanii waliopewa shavu ni Harmonize, Joeboy na Skibi huku ikiwa na nyimbo tano.

Baada ya kusajiliwa na lebo ya Konde Gang, Ibraah amekwisha toa nyimbo mbili ambazo ni “Nimekubali” pamoja na “Sawa.”

EP hiyo itafanya idadi ya kazi rasmi chini ya mwamvuli wa Konde Gang kuwa ya pili baada ya album ya Harmonize (Afro East) kutangulia mapema mwaka huu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey