Sambaza

Rosa Ree Aelezea Alivyokutana na Rayvanny, ‘Shika Ndinga Remix’

Rapa wa Tanzania Rosa Ree ameelezea ni namna gani walifanikiwa kufanya remix ya ngoma yake “Shika Ndinga” na Rayvanny.

Wimbo huo ulitayarishwa na  Bin Laden na remix yake imewapendeza mashabiki baada ya nyota Rayvanny kuweka mistari yake ya kuchana na imekuwa nzuri.

“Rayvanny aliniambia ameipenda akaniambia nimtume nikamtumia baadaye akanisikilizisha namna alivyoua nikapenda sana, tukakubaliana kufanya remix,” alisema Rosa Ree.

Hata hivyo wimbo huo umewekwa kwenye You Tube ya Rayvanny na Rosa Ree alipoulizwa kuhusu hili alijibu “hayo ni maamuzi ya uongozi.”

“Rayvanny ana wafuatiliaji wengi kwenye You Tube yake hivyo ulikaa na uogozi tukaamua kuweka kwa Rayvanny” aliongezea Rosa Ree.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey