Young Thug Asema Alikaribia Kufa, Figo na Mapafu Yalifeli
Young Thug amefunguka kuwa alipata matatizo ya figo na mapafu na madaktari walimuambia ana nafasi ndogo ya kupona.
Kwenye tamasha la mtandaoni la mwanamuziki mwenzake “Offset” Young Thug aliyazungumza hayo kwa kusema alilazwa na baada ya hapo ndiyo akajua ni mgonjwa haswa.
“Nililala kitandani tu kisha nikasema, jamani iteni gari la wagonjwa siwezi kujisogeza.” Alisema msanii huyo.
“Nilipofika hospitali ndiyo nikagundua ugonjwa huo na nilikuwa kama nimekufa tayari, nilikaa hospitali kwa siku 17,” aliongeza Young Thug.
Toa Maoni Yako Hapa