Sambaza

Diamond Azungumzia Ujio wa Album Yake Mpya

NYOTA wa Bongo Fleva Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ amesema kuwa hii hali iliyoikumba dunia ya janga la Corona imemfanya kuwekeza nguvu zake kwenye album yake mpya.

Mwanamuziki huyo ambaye siku za karibuni alitangaza kusaidia familia 500 za Tanzania kwa kuwalipia kodi amesema kwa sasa amepumzika nyumbani na hana shughuli nyingi za kufanya.

“Kwa sasa nimezoea kukaa nyumbani na kuwekeza nguvu zangu kwenye utengenezaji wa album yangu mpya ambayo itatoka hivi karibuni,” alisema nyota huyo.

“Janga la Corona limenifanya nione kuwa hatutaishi milele ndiyo sababu mimi na uongozi wangu tumeamua kuwasaidia watu wenye uhitaji wakati huu wa Corona,” aliongeza mkali huyo wa kibao cha ‘Kanyaga.’

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey