P Diddy: Sitampigia Kura Joe Bidden, Kisa Hatumpendi Trump
Nchini Marekani Uchaguzi upo njiani na msanii P Diddy amekuwa muwazi ni kitu gani kitamfanya asimpigie kura au ampigie kura mgombea urais kupitia chama cha Democratic Joe Bidden.
Kupitia mahojiano aliyofanya na mrembo Naomi Campbell mwishoni mwa mwezi Aprili, P Diddy alisema kuwa kura ya mtu mweusi ni ya gharama.
“Kura ya mtu mweusi haitaenda bure,” alisema rapa huyo. “Tutataka kuona ahadi, tunataka kujua ni nini tutapata kama malipo ya kura yetu kwa sababu hakuna kilichobadilika Marekani kwa watu weusi.”
“Hatuwezi kuchukulia hili suala kiurahisi na kumpigia kura kisa tu hatumpendi Trump au kisa watu weusi wanapaswa kuwa upande wa chama cha Democrat,” aliongeza P Diddy.
Toa Maoni Yako Hapa