Chameleone Azungumzia Kutokamilika Redio Yake
MWAKA 2018 msanii nguli wa Uganda, Jose Chameleone, alitangaza hadharani kuwa anapanga kuanzisha kituo cha redio ambacho kingeitwa “Chameleone FM.”
Aliyasema hayo wakati anatumbuiza kwenye tamasha la Saba Saba.
Alifichua kuwa anafanya hivyo ili kuupa muziki wa Uganda nafasi ya kutanua wigo zaidi.
“Tunapaswa kusaidia vya kwetu, kupenda vya kwetu, na kusukuma mbele vya kwetu, hivyo nitafungua kituo cha redio mwakani,” alisema msanii huyo mwaka 2018.
Miaka miwili sasa bado redio hiyo haijaonekana popote na kufanya mashabiki kuuliza juu ya ukweli wa kauli yake.
Akifanya mahojiano na Spark TV, msanii huyo alitoa ufafanuzi kwamba “tunaruhusiwa kuweka mipango, nilisema sababu vifaa vilikuwa tayari vimefika ila baadhi vilikuwa bado havijafika na ni ghali, hivyo hatukufanikisha. Tutaifungua kwenye muda sahihi.”